Ad Code

KITUO CHA TANO, SIMONI WA KIRENE ANAMSAIDIA YESU.

WIMBO

Kwa simon heri ya kweli, Mimi pia Yesu nisaidie kuchukua mzigo wa ukombozi Kuteswa, kuteswa pamoja naye.

KITUO CHA TANO.
Simoni wa Kirene anamsaidia Yesu.

Ee Yesu tunakuabudu, tunakushukuru.

Kwa Kuwa umewakomboa watu kwa msalaba Mtakatifu.

Nausifu ukarimu wa Simon wa Kirene.
Ee Bwana, unijalie ukarimu kama huo, nitie ushujaa kama huo, niitikie nami wito wa kukusadia kuchukua msalaba. Nitoe zaka na michango yote ya uenezaji wa dini; nijitolee mimi mwenyewe katika kazi ya maendeleo ya dini.
Uwajalie vijana wengi wito wa upadre, waweze kuchukua msalaba pamoja nawe kwa ajili ya wokovu wa dunia.
Uwaimarishe viongozi wa dini. Usitawishe moyoni mwa waamini wote mwamko wa utume.

Baba yetu…(×1)

Salamu Maria…(×1)

Atukuzwe Baba na..(×1)

K.We Bwana, utuhurumie….
W.Utuhurumie….

Roho za waamini wapate rehema kwa Mungu, wapumzike kwa amani.
Amina.

Post a Comment

0 Comments