Ad Code

KITUO CHA NNE, YESU ANAKUTANA NA MAMA YAKE.


WIMBO
Huko njiani we Maria waonaje hali ya mwanao ni damu tupu na vidonda Machozi, machozi yafumba macho.

KITUO CHA NNE.
Yesu anakutana na Mama yake.

Ee Yesu tunakuabudu, tunakushukuru.

Kwa kuwa umewakomboa watu kwa msalaba wako Mtakatifu.

Wote wawili Mama na mwanae wanaumia moyoni kwa ajili ya dhambi zangu.

Ee Yesu, Mwana wa Maria, unitilie moyoni mwangu upendo na Ibada kwa Bikira Maria, unijalie na ulinzi wake, nisitende dhambi tena.

Baba yetu…(×1)

Salamu Maria…(×1)

Atukuzwe Baba na…(×1)

K.Ee Bwana, utuhurumie…
W.Utuhurumie…

Roho za waamini wapate rehema kwa Mungu, wapumzike kwa amani.
Amina.


Post a Comment

0 Comments