WIMBO
Uso wa Yesu Malaika Betlehemu walikuabudu, Bahati yake Veronika Kupangusa, kupangusa mfalme wa mbingu.
KITUO CHA SITA.
Veronika anapangusa uso wa Yesu
Ee Yesu tunakuabudu tunakushukuru
Kwa Kuwa umewakomboa watu kwa msalaba wako Mtakatifu.
Mama huyu ni kinyume kabisa cha pilato.
Veronika anajua analopaswa kutenda na analitenda bila kujali macho na maneno ya makundi ya watu waovu.
Ee Yesu, uliyemtuza Veronika zawadi ya picha ya uso wako juu ya kitambaa, unijalie ushupavu na ujasiri wake wa kutenda mema, ili roho yangu ipambwe kwa chapa ya uungwana na utakatifu wako.
Baba yetu…(×1)
Salamu Maria..(×1)
Atukuzwe Baba na..(×1)
K.Ee Bwana, utuhurumie…..
W.Utuhurumie….
Roho za waamini wapate rehema kwa Mungu, wapumzike kwa amani.
Amina.
0 Comments