WIMBO
Wakimvuta huku na huku Wauaji wanamchokesha bure, Chini wamtupa bado kwa nguvu Aibu, aibu yao milele.
KITUO CHA SABA.
Yesu anaanguka Mara ya pili.
Ee Yesu tunakuabudu tunakushukuru
Kwa kuwa umewakomboa watu kwa msalaba wako mtakatifu.
Ee Yesu uliyelegea mno kwa mateso makali, unapoanguka mara ya pili kwa ajili ya udhaifu wa mwili, wanionya kwamba hata mimi naweza kurudi dhambini kwa udhaifu wa moyo.
Nipe basi neema ya kuepuka nafasi za dhambi na visa vyenye kunikwaza na kurudisha dhambini.
Baba yetu…(×1)
Salamu Maria…(×1)
Atukuzwe Baba na..(×1)
K.Ee Bwana, utuhurumie…
W.Utuhurumie…
Roho za waamini wapate rehema kwa Mungu, wapumzike kwa amani.
Amina.
0 Comments