WIMBO
Ona muumba mbingu na nchi, yupo chini mzingo wamwelemea na mtu kiumbe chake kwa ukali Ampiga, ampiga bila huruma.
KITUO CHA TATU.
Yesu anaanguka mara ya kwanza.
Ee Yesu tunakuabudu, tunakushukuru.
Kwa Kuwa umewakomboa watu kwa msalaba wako Mtakatifu.
Yesu amedhoofika sana, anaanguka chini, kisha anasimama, anaendelea na safari ya ukombozi.
Ee Yesu, uliyeanguka chini ya msalaba kwa ajili ya udhaifu, ukasimama tena; usiniache katika Tamaa nikianguka dhambini, bali nisimame mara moja, nikufuate.
Baba yetu…(×1)
Salamu Maria…(×1)
Atukuzwe Baba na…(×1)
K.Ee Bwana, utuhurumie….
W.Utuhurumie……
Roho za waamini wapate rehema kwa Mungu, wapumzike kwa amani.
Amina.
0 Comments