Ad Code

KITUO CHA KUMI NA TATU, YESU ANASHUSHWA MSALABANI

WIMBO

Mama Maria mtakatifu Upokee maiti ya mwanao, Tumemwua kwa dhambi zetu Twatubu, twatubu kwake na kwako.

KITUO CHA KUMI NA TATU.
Yesu anashushwa msalabani.

Ee,Yesu tunakuabudu tunakushukuru.

Kwa kuwa umewakomboa watu kwa Msalaba wako Mtakatifu.

Ee Yesu, uliyeshushwa msalabani baada ya kufa, unijalie nidumu katika maisha ya kujitoa sadaka mpaka siku ya kufa kwangu.

Nielewe na nikubali kwamba baada ya kufa ndio mwisho wa vita na mashindano ya Kikristo.

Baba yetu…(×1)

Salamu Maria…(×1)

Atukuzwe Baba na…(×1)

K.Ee Bwana, utuhurumie…..
W.Utuhurumie……

Roho za waamini wapate rehema kwa Mungu, apumzike kwa amani.
Amina.

Post a Comment

0 Comments