Ad Code

KITUO CHA KUMI NA MOJA, YESU ANASULIBISHWA MSALABANI

WIMBO

Hapo Mkristo ushike moyo Bwana wako alazwa msalabani Mara miguu na mikono Yafungwa, yafungwa kwa misumari.

KITUO CHA KUMI NA MOJA.
Yesu anasulibishwa msalabani.

Ee Yesu tunakuabudu, tunakushuru.

Kwa kuwa umewakomboa kwa msalaba wako mtakatifu.

Ee Yesu uliyepigiliwa misumari msalabani, nakutolea akili na utashi wangu, vifungwe pamoja na miguu yako, nipate kuwaza, kusema na kutenda siku zote yale tu yanayolingana na utukufu wa msalaba wako mtakatifu.

Ee Yesu, mimi ni mfungwa wako. Nisadie kuimarisha kifungo hicho kwa sala, sakramenti na fadhila za Kikristo.

Baba yetu…(×1)

Salamu Maria…(×1)

Atukuzwe Baba na…(×1)

K.Ee Bwana, utuhurumie…
W.Utuhurumie…

Roho za waamini wapate rehema kwa Mungu, wapumzike kwa amani.
Amina.

Post a Comment

0 Comments